Ngoja leo nikupe hiki kisa cha Abby ambaye alikuwa mwanamke mchapakazi sana, na mfanyakazi muhimu katika kampuni kubwa ya mawasiliano huko Kigoma. Alikuwa akijitolea muda wake wote na kufanya kazi kwa bidii isiyo na kifani. Mara kwa mara, aliongoza miradi migumu na alikuwa akipata sifa nyingi kutoka kwa wakubwa wake kwa utendaji wake bora.
Hata hivyo, licha ya utendaji wake mzuri, Abby alikaa miaka minne bila kupandishiwa mshahara hata senti moja. Wenzake, ambao hata hawakufanya kazi kwa bidii kama yeye, walipata nyongeza na kupandishwa vyeo, lakini Abby kila mara alikwama pale pale. Alijaribu kuomba nyongeza mara kadhaa, akieleza jinsi alivyochangia katika mafanikio ya kampuni, lakini kila wakati alikataliwa kwa visingizio mbalimbali.…CONTINUE READING