Miaka kadhaa nyuma, Manecky alikuwa kijana mchangamfu, mwenye heshima, na mfanyabiashara mdogo mwenye juhudi jijini Mtwara. Alikuwa na kila sifa njema, lakini katika ulimwengu wa mapenzi, nyota yake ilionekana kuzama kabla hata haijawahi kung’aa. Kila uhusiano aliouanzisha uliishia kwa maumivu, na cha kushangaza, kila mara alikuwa anaachwa na mpenzi wake bila sababu ya msingi.
Mpenzi wake wa kwanza, Neema, alimtema siku moja tu baada ya Manecky kumnunulia zawadi ya gharama kubwa, akisema: “Samahani, Manecky. Sijui niseme nini, lakini nimeamua niondoke. Siyo wewe, ni mimi.” Kauli hii ya kizushi ikawa kama wimbo wa taifa katika maisha yake ya kimapenzi.…CONTINUE READING