Biashara ikashamiri kuliko zote za awali

Kutana na Mohamed, kijana aliyekulia Katavi, alikuwa na ndoto kubwa za kuwa mfanyabiashara maarufu. Tangu akiwa mdogo, aliamini kwamba njia ya kumtoa kwenye umasikini ni kujituma, kuwa mbunifu, na kuanzisha biashara zake mwenyewe. Hakuwa mtu wa kukata tamaa, na kila mara alipoona nafasi, aliitumia kwa nguvu zote. Lakini licha ya juhudi zake zote, Mohamed alikumbana na kitu ambacho kilimchanganya zaidi ya chochote—biashara zake hazikuwahi kudumu.

Biashara ya kwanza aliyowahi kufungua ilikuwa ya kuuza vifaa vya simu. Aliwekeza kila senti aliyokuwa ameokoa kwa miaka miwili. Siku za mwanzo mambo yalionekana kwenda vizuri, lakini baada ya muda mfupi wateja wakapungua ghafla. Akapata hasara kubwa na kulazimika kufunga duka. Alisema pengine ni bahati mbaya.…CONTINUE READING