Happy ni jina la binti mrembo kutoka Manyara, lakini kinyume cha jina lake, maisha yake ya siri yalikuwa yamejaa huzuni na mashaka. Macho yake yalikuwa angavu kama Almasi, na tabasamu lake liliweza kuyeyusha barafu, lakini ndani ya moyo wake alikuwa akihifadhi siri nzito iliyotesa uhusiano wake na mpenzi wake, Ben.
Ben alikuwa mwanaume mwema, mchapakazi, na aliyempenda Happy kwa dhati. Walifunga ndoa kwa shamrashamra, wakiamini wamepata kipande cha Pepo hapa duniani. Hata hivyo, mara tu walipoingia kwenye maisha yao ya pamoja, Happy aligundua changamoto iliyoficha uso wake. Katika uhusiano wao wa faragha, Happy hakuweza kupata hisia zozote za tendo la ndoa. Alijisikia mtupu, baridi, na asiye na uhai. Ilikuwa kama sehemu muhimu ya uke wake ilikuwa imezimwa.…CONTINUE READING