Salmu, kijana mwenye miaka 27 kutoka Kariakoo, alikuwa akijulikana kwa juhudi na mwendo wake wa haraka katika mitaa ya biashara. Alijipatia riziki kwa kuuza nguo za mitumba, akiweka mabunduki yake ya mzigo kila alfajiri kwenye kona ya soko maarufu kwa wateja wengi. Hata hivyo, licha ya juhudi zake na muda mwingi aliowekeza, biashara yake ilikuwa haipigi hatua. Kila mwisho wa wiki alipofanya hesabu, aligundua amepoteza zaidi kuliko alichopata.
Wakati wenzake walipata faida kubwa kutokana na mzigo ule ule, Salmu alijikuta akiwa na nguo zilizooza, kukosa wateja, au kukumbwa na hasara isiyoelezeka. Wakati mwingine mzigo wake ulipokuwa mzuri, wateja waligeuka na kuelekea kwenye mabanda ya jirani. Alianza kuamini kuwa pengine bahati haikuwa upande wake.…CONTINUE READING